Jumatano, 26 Oktoba 2016

YANGA YAIVURUGA JKT RUVU

Siku moja baada ya kocha mkuu wa Dar es salaam young Africa kujiuzulu leo hii likizo hicho kimeondoka na ushindi wa goli nne kwa bila dhidi ya JKT RUVU maafande hawa toka mkoani pwanii. Shukrani zimwendee obrey chirwa aliendelea kuzifumania nyavu pia supersub amisi tambwe akiingia kipindi cha Pili akifunga magoli mawili na saimon msuva akafunga moja.Kwa mchezo huyo simba wanaongoza kwa pointi 29 yanga wanafuatia kwa point 24..

VIKWAZO VYA UJASILIAMALI

Ujasiliamali ni nguzo muhimu katika maendeleo ya watu Popote duniani. Hii ni sekta muhimu ambayo inawezakuleta ajira ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja kwa watu hasa vijana. Kwa Nchi zinazoendelea hasa za Africa sekta hii ni muhimu sana ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Nchi nyingi za Africa ina namba kubwa ya vijana wasio na kazi ambapo hupelekea vijana kujiunga na delta zisizo rasmi ili wapate pesa za haraka na kukidhi mahitaji Yao. Je ni nini changamoto zinazowakabili?
  • Kukosekana.kwa mitaji: hili ni.tatizo sugu amabalo hufanya watu wengi washindwe kwenye sekta ya ujasiliamali. Bank na taasisi za kifedha zimekuwa zinatoa masharti magumu ili kupata Mtaji kama uwe na kiwanja ,nyumba na kadhalika.
  • Elimu duni ya ujasiliamali inachangia wale wanothubutu kushindwa kufikia malengo au mafanikio kwa sababu ya elimu duni au mazoea pia ugumu wa maisha hupelekea biashara kutofanikiwa.
  • Starehe vijana wengi wanakumbwa na nanga la.kupenda starehe hivyo hupelekea kipato kuishi kwenda kumbi za starehe , bar na kwenye majumba ya kulala wageni

Jumatano, 12 Oktoba 2016

CHANGAMOTO ZA KILIMO KWA WAKULIMA

Tanzania ni Nchi iliyojaliwa mabonde na ardhi yenye rutuba. Nchi ambayo ina mito mingi mikubwa kama rufiji,malalasi,ruaha n.k pia kuna maziwa makubwa kama Victoria,Nyasa na Tanganyika, hivyo inawezekana kwa kiasi kikubwa shughuli za kilimo zikafanyika mwaka Mzima. Ila wakulima wamekuwa wakipata changamoto nyingi sana ambazo ni:-

  • PEMBEJEO KUCHELEWA AU KUKOSEKANA
      Wakulima wamekuwa wakisotea kupata pembejeo toka serikalini ambapo kwanza hazifiki kwa wakati na zikifika zinakuwa chache kiasi kwamba watu wachache ndo wanaopata. Hili limeshamili sana vijijini huko ambapo wananchi wanalalamika sana suala hili
  • UKOSEFU WA SOKO LA MAZAO
Bei ya mazao imekuwa gonjwa sugu kwani wanunuzi  wamekuwa wakijipangia bei ya kununua mazao bila kujali upande wa mkulima. Hili suala linapelekea mpaka wakulima wanakata tamaa ya kulima mashamba makubwa wakihofia hasara ambayo wanaweza kupata.  Bado matumizi ya jembe la Mkono yanaendelea na kilimo cha kisasa watu wachache sana ndo wanafanya. Hii hupelekea mavuno machache na mazao yasiyo bora.
  • MATUMIZI YA ZANA DUNI ZA KILIMO

Jumamosi, 4 Juni 2016

BONDIA BINGWA WA MIAKA YA 60 AFARIKI DUNIA

Aliyeluwa bondia wa kwanza maarufu mweney asili ya Kiafrika, Muhammud Ali, wa Marekani amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.
Kulingana na msemaji wa familia yake, bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu, anayejulikana sana kote duniani kwa sababu ya machachari yake katika ngumi, alifariki katika jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.
Alikuwa na matatizo ya kupumua, hali ambayo ilitatanishwa zaidi na maradhi ya Parkinson, ambayo ni hali ya mgonjwa kutetemekatetemeaka.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa ibada ya mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky.

Jumamosi, 30 Aprili 2016

MATOKEO LIGI KUU VODACOM LEO TAREHE 30/05/2016

Mabingwa Watetezi na Vinara wa VPL, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Yanga Leo wamezidi kujongomea juu kileleni baada ya kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Toto African 2-1 huko CCM Kirumba, Mwanza.
Toto walitangulia kuifunga Yanga kwa Bao la Dakika ya 39 la William Kimanzi na Yanga kupiga Bao 2 Kipindi cha Pili Dakika za 50 na 78 Wafungaji wakiwa Deus Kaseke na Juma Abdul.
Ushindi huu umeifanya Yanga izidi kupaa kileleni ikiwa na Pointi 65 kwa Mechi 26 ikifuatiwa na Azam FC yenye Pointi 58 na Simba 57  ambao wamecheza Mechi 25 na Kesho Jumapili wanapambana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZAHARIBU MIUNDOMBINU YA BARABARA

Kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara zimesababisha wasafiri wanaofanya safari kati ya wilaya ya Tandahimba, Newala, na Dar es Salaam kupata adha kubwa ya usafiri kutokana na barabara kuharibika na kulazimika Magari kuvutwa na Scaveta zinazofanya kazi ya kupunguza mlima kinombedo uliopo wilaya ya Tandahimba.
Wakiwa katika jitihada za kuvuka mlima Kinombedo ambao licha ya kuwepo kwa lami udongo unaoporomoka kutoka juu ya mlima huo umekuwa ukisababisha utelezi na magari kushindwa kupanda mlima ambapo awali madereva wanaoendesha mashine za kuchimbia udongo walishindwa kutoa msaada na kulazimu madereva kuanza kuchimba barabara hali ambayo ilisababisha foleni kubwa zaidi kutokana na malori kuziba njia.
Baada ya jititihada zao kugonga mwamba na kusababisha foleni ya malori ya mizigo pamoja na mabasi ya abiria, Kampuni inayopunguza mlima chini ya msimamizi wake Bw. Haji Abubakari ambaye hakutaka kutaja jina la kampuni inayofanya kazi ilitoa msaada wa kuyavuta magari hayo ambayo baadaye yaliendelea na safari zake , Lakini bwana Haji amesema eneo hilo linapunguzwa mlima ili kuwezesha magari kupita kwa urahisi.
Wakiongea na Safari redio baadhi ya madereva wanaofanya safari zao kati ya Wilaya ya Tandahimba, Newala na Dar es Salaam wameilalamikia serikali ya Mkoa kwa kushindwa kujenga barabra hiyo kwa kiwango cha lami licha ya kuwa imekuwa ina uhitaji mkubwa kwa wananchi wanaoishi na wanaosafiti katika wilaya hizo.
Mmoja wa madereva hao aliyejitambulisha kwa jina na Charles Paulo amesema mara nyingi kipindi cha mvua kumekuwa kukijitokeza kero ya uharibifu wa barabara ambayo kwa namna moja au nyingine imekuwa ikichangia uchakavu wa vyombo vya moto ambavyo vimekuwa vikipita katika barabara hiyo.
Wiki iliyopita Serikali kupitia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisema imetenda fedha zaidi ya shilingi Milion 1000 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya barabara na kujenga kwa kiwango cha lami barabara inayounganisha Mkoa wa Mtwara na Viunga vyake.Kuhu ikidai kuwa serikali kupitia wakala wa barabara Tanroads tayari imesaini mkataba na mkandarasi kutoka Botswana.

AINA ZA WANAWAKE MICHEPUKO

  1. MCHEPUKO LAMI: Huu ni ule ambao hauombi pesa, katulia hana mapepe, uwe naye au usiwe naye maisha yake yanaendelea tu.
  2. MCHEPUKO VUMBI: Huu ni ule wa vibomu!! mara ooohhh sina pesa, naomba vocha, sijui simu imekufa, oooh mara nipo saluni nadaiwa elf thelathin, naomba nauli…..n.k! Na hii ndio noma maana njia kuu lazima washtuke mana mchepuko vumbi unachafua na unasumbua full time
  3. MCHEPUKO KOKOTO: Huu ni mkali zaidi ya njia kuu maana kila mara huuliza upo wapi, Uko na nani, why hupokei simu yangu? Kama uko kwako naomba utoke nje tuongee kidogo na leo uwe na mimi tu…Yaani tabu tupu! MCHEPUKO MATOPE: Yaani huu usiombe hata kukutana nao maana wenyewe ndio fu
  4. nga kazi.. Huu bana unajua kuchuna hasa ila pale unapoupa pesa na wenyewe unaenda kuzihonga zote kwa mchepuko wake mwingine yaani hatari tupu

Alhamisi, 28 Aprili 2016

MATOKEO UEROPA LIGI MECHI ZA NUSU FAINALI

Shakhtar Donesk (ukraine) wamesulu na sevilla (spain) kwa magoli mawili kwa mawili na kujiweka katika nafasi mbaya ya kusonga mbele kwa hatua ya fainali pale Arena Lviv. Kwa matokeo hayo basi shakhtar donesk wanahitaji ushindi wowote nchini spain alhamisi ijayo ili wafuzu kwenda fainali au suluhu ya magoli kuanzia matatu ili wakate tiketi ya fainali


Majogoo wa Jiji liverpool washindwa kutamba Huko spain baada ya kukubali kipigo cha Goli moja toka kwa villareal ya spain katika Nusu fainali ya Kwanza  huko nchini spain. Iliwachukua Villareal dakika 91 kupata goli la ushindi lililopachikwa kimiani na Lopez Adrian pale stadium el madrigal na kujiwekea mazingira mazuri kwenye mchezo wa pili utakaopigwa Anfield Alhamisi ijayo.
Watu wengi husindwa kubana matumizi kutokana na kukosa elimu ya jinsi ya kutumia pesa. Baadhi wamesoma na wengine wanaendelea kusoma masomo mbalimbali yanayohusu pesa na wanahitimu vizuri, lakini wanapokuja katika uhalisia wa maisha wanajikuta wanafeli vibaya kutokana na kutoutambua umuhimu wa kuwa na nidhamu ya pesa.
Msomaji wangu nikupe dondoo kadhaa ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukusaidia katika kubana matumizi na hatimaye hata kama kipato chako ni kidogo, kikakidhi mahitaji yako muhimu na pia kukawepo na ziada.
Usipendelee kukopa
Kuna watu wengi sana wanaishi kwa kukopa kopa vitu madukani na kwa watu. Mtindo huu ni mbaya sana kwa ukadiriaji wa matumizi, kwani haumtii uchungu mkopaji hadi pale atakapokuwa analipa. Mara nyingi ukopaji huongeza gharama, hivyo inashauriwa ukiwa na 5,000 itumie hiyo, bila kutafuta ziada kwenye deni.
Kuwa na bajeti ndogo
Katika maisha pendelea kupanga bajeti yako kwa mafungu madogo madogo hasa ya wiki. Usivuke mipango hiyo kwa kutumia bajeti ya wiki inayofuata.
Usitembee na pesa nyingi
Baadhi ya watu wanapenda kutembea mitaani huku wakiwa na pesa nyingi mifukoni. Fahamu kuwa kutembea na pesa usizozipangia bajeti utajikuta unashawishiwa kuzitumia bila mpango.
Hata hivyo, unashauriwa kujenga tabia ya kukaa nyumbani na familia yako na kama utatoka siku za mwisho wa wiki basi weka bajeti ya kiasi ambacho utakitumia. Kitendo cha kutoka huku ukiwa na fedha nyingi kwenye pochi lako ni kujishawishi kufanya matanuzi yasio na msingi.
Epuka kununua vitu kwa rejareja!
Unapopata mshaara wako au unapofikiria kuhusu matumizi ya nyumbani kwako pendelea sana kununua vitu kwa jumla ambavyo utavitumia kwa mwezi mzima. Epuka kununua vipimo vidogo vidogo kwani vinaumiza na kuvuruga bajeti.

Pika chakula nyumbani kwako
Watu wengi hasa vijana wanapenda sana kula kwenye migahawa na hotelini. Ulaji huu ni ghali, hivyo inashauriwa kila mtu ajipikie chakula chake nyumbani. Hii itamsaidia kutumia pesa kidogo katika suala la chakula.

Ifundishe familia nidhamu ya pesa
Kuna watu hawawafundishi watoto na wake zao nidhamu ya matumizi ya pesa. Mume/mke asinunue vitu ambavyo familioa haikuzitengea bajeti na asiwepo mtumia hovyo vitu vilivyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Akiba na mipango ni muhimu
Familia lazima ijiwekee akiba benki. Utunzaji wa pesa nyumbani si wa salama na mara nyingi hushawishi matumizi. Aidha unapoweka feda benki ziwekee malengo amambo utakuwa ukiyatimiza taratibu si mpaka pesa hizo ziwe nyini.

Kuwa na familia ndogo
Ingawa ni hali halisi ya maisha ya kiafrika kwa familia moja kuwa na watu wengi lakini inashauriwa kwamba, ili kupata ziada ya kipato lazima familia iwe ndogo, vinginevyo mshahara wote unaweza kutumika kwa chakula tu. La kama familia itakuwa ni kubwa basi kila mmoja afanye kazi ili uwepo usaidianaji wa kuendesha familia

FAIDA ZA KUJIAJIRI MWENYEWE





1. Ni njia bora ya kukufikisha kwenye uhuru wa fedha.
Inawezekana ukawa umechoka na kazi unayoifanya na unaoina haifai kwa namna moja au nyingine. Lakini njia bora ya kuweza kuondokana na utumwa huo ambao unakukabili ni kuanzisha biashara yako mwenyewe ambayo utaisimamia mpaka ikuletee mafanikio unayoyahitaji.

2. Ni Njia bora ya kujifunza.
Hakuna njia bora ya kujifunza kuhusu kutunza na kumiliki pesa kama biashara. Hili ndilo eneo  ambalo utajifunza mengi kuhusu masoko, namna ya kukuza mtaji na jinsi ambavyo unaweza ukaufikia uhuru wa kipesa. Kwa hiyo kama una biashara yako inakusaidia kujifunza yote hayo hatua kwa hatua.

3. Ni njia bora yakujifunza kujitegemea.
Unapokuwa kwenye ajira kwa kawaida unakuwa unamtegemea mtu fulani ambaye ndiye akuamulie juu ya maisha yako. Lakini kwenye biashara mambo hayako hivyo. Wewe ndiye unakuwa mwamuzi mkubwa wa maisha yako. Na unakuwa unakikisha unafanya kila linalowezeka mpaka biashara yako ifanikiwe.

4. Inakuwa inakupa hamasa ya mafanikio zaidi.
Huo ndiyo ukweli unaotakiwa ujue kuwa, unapokuwa na biashara inakuwa inakupa hamasa ya kuweza kufanikiwa na kusonga mbele zaidi. Tofauti na ajira ni rahisi kusema kuwa ‘aaah kazi yenyewe siyo yangu kwanza’ kwa hiyo unakuwa unafanya kwa jinsi unavyojisikia. Lakini kwenye biashara mambo hayako hivyo ni lazima kujituma ili kufanikiwa.

5. Inakuongezea ujasiri.
Unapokuwa mfanyabishara ni hatua nzuri sana kwako ya kukupelekea kuwa na ujasiri wa hali ya juu. Hiyo yote ni kwa sababu unapofanikiwa katika biashara moja unakuwa ndani yako una hamasa kubwa ya kutaka kufanya biashara nyingine tena kwa mafanikio. Kwa hali hiyo unakuwa una maamuzi mengi ya kijasiri ambayo ni rahisi kukusaidia kukusonga mbele.

6. Ni njia rahisi ya kufuata mipango na malengo yako.
Mara unapoanzisha biashara yako unakuwa upo kwenye njia sahihi ya kufuata ndoto za maisha yako. Hii yote ni kwa sababu unakuwa unakifanya kile kitu ambacho unakipenda kwa dhati toka moyoni mwako. Wakati unapokuwa kwenye ajira unakuwa unafanya tu ilimradi mkono uende kinywani. Hiyo ndiyo faida kubwa mojawapo ya kuwa kwenye biashara.

7. Inakufanya unakuwa ni mtu wa vitendo.
Watu wengi mara nyingi ni waongeaji bila ya kuwa watu wa vitendo. Lakini kitendo cha kuwa na biashara yako mwenyewe inakupelekea unakuwa ni mtu wa vitendo. Utaelewa vizuri umuhimu wa kuchukua hatua katika biashara tofauti na ambavyo ungekuwa hufanyi biashara ingekupelekea wewe kuwa na maneno mengi bila utekelezaji.

8. Ni njia bora ya kufanya mambo mengine zaidi.
Unapokuwa kwenye biashara inakuwa ni njia bora ya kufanya mambo mengine bora zaidi. Kama ulikuwa una lengo moja na umelikamilisha inakuwa ni rahisi kuweza kulifatilia lengo lingine mpaka tena kulifanikisha. Na hiyo nguvu yote ya kufanya mambo mengine inakuja kutokana na ujasiri ambao tayari unakuwa umeshajijengea kwenye biashara yako.

FAIDA YA WANAWAKE WANENE

Wepesi wa kusamehe 

Mwanamke mnene mara nyingi huwa ni mwepesi wa kusamehe pale anapokwazwa na mtu; hapendi kuweka vinyongo moyoni.

Wanapenda kuomba radhi

Wataalamu wa mahusiano wanasema wanawake wenye maumbo makubwa wanasifa ya kuomba radhi pale wanapokosea.

Wanatulia kwa mwanaume mmoja

Takwimu zinaonesha wanawake wanene sio viruka njia; mara nyingi hutulia katika mahusiano na kudumu na mwanaume mmoja kwa kipindi kirefu.

Wakipenda wanapenda kweli

Wanawake wanene wanatabia ya kupenda kwa dhati mara wanapoingia katika mahusiano; watu hawa husifika kwa kuwa na mapenzi ya dhati kwa wapenzi wao.

Sio wabishi

Wanawake wanene hawana silka ya ubishi, inasemekana wanawake wembamba ndio wenye tabia ya ubishi lakini kwa upande wa wanawake wanene hawana tabia ya mabishano na hawapendi kujiingiza katika ubishi.

Watiifu

Kwa asili yao wanawake wanene ni wanyenyekevu na watiifu kitu ambacho si rahisi kukuta kwa kila mwanamke. Bila shaka utii wao ndio unaowasaidia katika kudumisha mahusiano yao.

Hawaringi sana

Inasemekana wanawake wenye maumbile makubwa hawana tabia ya kujivuna wala kujikweza wanauwezo wa kuishi na watu wa aina yoyote kwa sababu ya unyenyekevu walionao.

Wanajua kudeka na kudekeza

Wataalamu wa mahusiano wanasema kwa asili wanawake wenye miili mikubwa wanapenda kudeka na kudekezwa katika mapenzi; kwa kufanya hivyo hujikuta wakidumu kwa kipindi kirefu katika mahusiano yao.

Vizazi vyao vinaakili timamu

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wataalamu wa afya umebaini wanawake wenye maumbo makubwa huzaa watoto wenye akili nyingi.

Wanasahau haraka 

Moja ya hasara walionayo wanawake wanene ni tabia ya kusahau mambo kwa haraka. yawezekana hali hii huwapata kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kutuna kumbukumbu.

Jumatano, 27 Aprili 2016

EUROPA CUP SEMI FINALS TODAY CONTINUES

Mashindano ya vilabu Huko ulaya yataendelea tena leo usiku. Villarreal watawakaribisha majogoo wa jiji Liverpool katika nusu fainali huko estadio  el Madrigal jijin valencia wakati wahispania weingine sevilla watakuwa nchini ukraine kupambana na shaktar donesk katika nusu fanaili ya kwanza.. Sevilla anasaka ubingwa wa tatu mfululizo wakati Liverpool wakijaribu na kujipambanua kusaka Ubingwa huo baada ya ukame wa mataji kwa  Muda mrefu

MATOKEO LIGI YA MABINGWA YA ULAYA ATLETICO MADRID VS BAYERN MUNICH

Uefa champion League iliendelea jana usiku ikiwakutanisha Atletico Madrid (SPAIN) na Mianmba ya Ujeruman Bayern Munich pale Vicente Calderon ambapo mchezaji sauli wa Atletico Madrid aliwainua washabiki wa Atletico na kuipa timu yake goli la ushindi katika kipindi cha kwanza. Hivyo kwa matokeo hayo Atletico wanatanguliza mguu mmoja kwenye Fainali itakayocheza huko Millan mwezi May..

MTWARA TUIOTAYO NA MTWARA TULIOITAKA



Habari ndugu wasomaji
Ni miaka Kadhaa imepita Tangu serikali itangaze kugundulika kwa gesi huko Mnazi bay Mtwara. Kugundulika kwa gesi kulivuta hisia kutokana na ukweli kwamba kusini kulioneka hakuna chochote kinachoingizia pao la taifa ukilinganisha na mikoa ya Mwanza, Arusha ambayo ilikuwa na Madini.Nao wananchi wa  Mtwara walifurahi kuona sasa ni wakati wao wa kuneemeka kutoka na gesi. Baada ya serikali kufanya upembuzi yakinifu ukapitisha swala la kupeleka gesi Dar es salaam kwa ajiri ya matumizi ya viwandani na kufua umeme kwani jiji hilo linalokabiliwa na uhaba wa umeme ilihari umeme wa maji toka vyanzo vingi umepelekwa dar es salaam. Hili lilizusha hasira kwa wananchi wa Mtwara  kwani walidhani kwamba mtwara wataachwa masikini na hawatanufaika na chochote. kilichotokea sitaki nikumbushe uchungu kwa wanamtwara na wapenda maendeleo ila tuu tuwaombee wapumzike salama waliotangulia mbele ya haki kutoka na hili swala.
siasa kwa upande wake ilichukua mkondo wanasiasa na wanapropaganda wakasema ooh mtwara watapata mafanikio kuna viwanda vingi vitajengwa kuna mahoteli kibao yatajengwa na mengine mengi ikiwa na kuwasomesha vijana pale veta mtwara kwenye fani ya gesi na mafuta na wengine walichukuliwa wakapelekwa chuo fulani wakasomee gesi na kuahidiwa ajira kabisa..Lilikuwa jambo zuri sana kwa mtizamo wa karibu ila kwa mtizamo wa mbali hmmm mashaka yalikuwapo.
Leo tumeshuhudia mengi sana yakifanyika mtwara hasa mahoteli kujengwa, majengo mengi yapo yamejengwa, kiwanda kikubwa cha cement kimejengwa ni mabadiliko makubwa ila kutokana na yote haya jee yameangalia mwananchi wa msijute au nambudi kule newala, Mkotokuyana nachingwea jee ananufaika na nin kutokana na hivi. cement dar es salaam 11000-12000/= tsh Nambudi-newala mtwara 14000-15000/= tsh, Ajira vijana wanaapply wa toka kusini but hata kwenye interview hakuna, waliosomeshwa kwenye gesi na mafuta ndo kwanza wanaambiwa wasome Zaidi angalau watapata ajira. korosho makato kibao na malipo ya pili wengine hawajapata jee huko hotelini wataingia kina nani na hizo nyumba wamejengewa watumishi serikali tuu. 
   nashukuru kwa muda na wakati wako
                              Mkulima toka Mnacho

MATOKEO YA YANGA LEO TAREHE 27/8/2016

Young african sports club watoto wa jangwan almaarufu "wakimataifa" wameendeleza ushindi kwa kuwafunga mgambo jkt ya Tanga goli mbili kwa moja, shukran zimwendee Daud kaseke aliyesawazisha bao baada ya Mgambo Jkt kuongoongoza.. Alikuwa kaseke tena aliipatia yanga Goli la pili na La ushindi.Kwa matokeo hayo young aftican wanaongoza ligi kuu kwa point 62 wakifuatiwa  na Azam fc wenye point 58,simba sc ni ya Tatu..

MAISHA CLUB INTER COLLEGE BASH NDANI YA MTWARA (gas city) TAREHE 29 APRIL 2016

ladies and gentlemen wa mtwara yote nikimaanisha TIA, STEMMUCO, UTUMISHI, na vyuo vyote ndani ya gas city usikose INTER COLLEGE BASH ndani ya Maisha club kwa mtonyo wa buku ten tuu yaan.. unaanzaje kukosaa