Aliyeluwa bondia wa kwanza maarufu
mweney asili ya Kiafrika, Muhammud Ali, wa Marekani amefariki leo
asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.
Kulingana na msemaji wa familia
yake, bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu, anayejulikana sana kote
duniani kwa sababu ya machachari yake katika ngumi, alifariki katika
jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.
Alikuwa
na matatizo ya kupumua, hali ambayo ilitatanishwa zaidi na maradhi ya
Parkinson, ambayo ni hali ya mgonjwa kutetemekatetemeaka.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa ibada ya mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni