Jumatano, 27 Aprili 2016

MTWARA TUIOTAYO NA MTWARA TULIOITAKA



Habari ndugu wasomaji
Ni miaka Kadhaa imepita Tangu serikali itangaze kugundulika kwa gesi huko Mnazi bay Mtwara. Kugundulika kwa gesi kulivuta hisia kutokana na ukweli kwamba kusini kulioneka hakuna chochote kinachoingizia pao la taifa ukilinganisha na mikoa ya Mwanza, Arusha ambayo ilikuwa na Madini.Nao wananchi wa  Mtwara walifurahi kuona sasa ni wakati wao wa kuneemeka kutoka na gesi. Baada ya serikali kufanya upembuzi yakinifu ukapitisha swala la kupeleka gesi Dar es salaam kwa ajiri ya matumizi ya viwandani na kufua umeme kwani jiji hilo linalokabiliwa na uhaba wa umeme ilihari umeme wa maji toka vyanzo vingi umepelekwa dar es salaam. Hili lilizusha hasira kwa wananchi wa Mtwara  kwani walidhani kwamba mtwara wataachwa masikini na hawatanufaika na chochote. kilichotokea sitaki nikumbushe uchungu kwa wanamtwara na wapenda maendeleo ila tuu tuwaombee wapumzike salama waliotangulia mbele ya haki kutoka na hili swala.
siasa kwa upande wake ilichukua mkondo wanasiasa na wanapropaganda wakasema ooh mtwara watapata mafanikio kuna viwanda vingi vitajengwa kuna mahoteli kibao yatajengwa na mengine mengi ikiwa na kuwasomesha vijana pale veta mtwara kwenye fani ya gesi na mafuta na wengine walichukuliwa wakapelekwa chuo fulani wakasomee gesi na kuahidiwa ajira kabisa..Lilikuwa jambo zuri sana kwa mtizamo wa karibu ila kwa mtizamo wa mbali hmmm mashaka yalikuwapo.
Leo tumeshuhudia mengi sana yakifanyika mtwara hasa mahoteli kujengwa, majengo mengi yapo yamejengwa, kiwanda kikubwa cha cement kimejengwa ni mabadiliko makubwa ila kutokana na yote haya jee yameangalia mwananchi wa msijute au nambudi kule newala, Mkotokuyana nachingwea jee ananufaika na nin kutokana na hivi. cement dar es salaam 11000-12000/= tsh Nambudi-newala mtwara 14000-15000/= tsh, Ajira vijana wanaapply wa toka kusini but hata kwenye interview hakuna, waliosomeshwa kwenye gesi na mafuta ndo kwanza wanaambiwa wasome Zaidi angalau watapata ajira. korosho makato kibao na malipo ya pili wengine hawajapata jee huko hotelini wataingia kina nani na hizo nyumba wamejengewa watumishi serikali tuu. 
   nashukuru kwa muda na wakati wako
                              Mkulima toka Mnacho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni