Tanzania ni Nchi iliyojaliwa mabonde na ardhi yenye rutuba. Nchi ambayo ina mito mingi mikubwa kama rufiji,malalasi,ruaha n.k pia kuna maziwa makubwa kama Victoria,Nyasa na Tanganyika, hivyo inawezekana kwa kiasi kikubwa shughuli za kilimo zikafanyika mwaka Mzima. Ila wakulima wamekuwa wakipata changamoto nyingi sana ambazo ni:-
- PEMBEJEO KUCHELEWA AU KUKOSEKANA
Wakulima wamekuwa wakisotea kupata pembejeo toka serikalini ambapo kwanza hazifiki kwa wakati na zikifika zinakuwa chache kiasi kwamba watu wachache ndo wanaopata. Hili limeshamili sana vijijini huko ambapo wananchi wanalalamika sana suala hili
Bei ya mazao imekuwa gonjwa sugu kwani wanunuzi wamekuwa wakijipangia bei ya kununua mazao bila kujali upande wa mkulima. Hili suala linapelekea mpaka wakulima wanakata tamaa ya kulima mashamba makubwa wakihofia hasara ambayo wanaweza kupata. Bado matumizi ya jembe la Mkono yanaendelea na kilimo cha kisasa watu wachache sana ndo wanafanya. Hii hupelekea mavuno machache na mazao yasiyo bora.
- MATUMIZI YA ZANA DUNI ZA KILIMO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni