Jumamosi, 4 Juni 2016

BONDIA BINGWA WA MIAKA YA 60 AFARIKI DUNIA

Aliyeluwa bondia wa kwanza maarufu mweney asili ya Kiafrika, Muhammud Ali, wa Marekani amefariki leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 74.
Kulingana na msemaji wa familia yake, bingwa huyo wa zamani wa uzani wa juu, anayejulikana sana kote duniani kwa sababu ya machachari yake katika ngumi, alifariki katika jiji la Phoenix Arizona, baada ya kulazwa hospitalini Alhamisi.
Alikuwa na matatizo ya kupumua, hali ambayo ilitatanishwa zaidi na maradhi ya Parkinson, ambayo ni hali ya mgonjwa kutetemekatetemeaka.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa ibada ya mazishi itafanywa nyumbani kwake Lousville, Kentucky.