Jumamosi, 30 Aprili 2016

MATOKEO LIGI KUU VODACOM LEO TAREHE 30/05/2016

Mabingwa Watetezi na Vinara wa VPL, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Yanga Leo wamezidi kujongomea juu kileleni baada ya kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Toto African 2-1 huko CCM Kirumba, Mwanza.
Toto walitangulia kuifunga Yanga kwa Bao la Dakika ya 39 la William Kimanzi na Yanga kupiga Bao 2 Kipindi cha Pili Dakika za 50 na 78 Wafungaji wakiwa Deus Kaseke na Juma Abdul.
Ushindi huu umeifanya Yanga izidi kupaa kileleni ikiwa na Pointi 65 kwa Mechi 26 ikifuatiwa na Azam FC yenye Pointi 58 na Simba 57  ambao wamecheza Mechi 25 na Kesho Jumapili wanapambana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni