Kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara zimesababisha
wasafiri wanaofanya safari kati ya wilaya ya Tandahimba, Newala, na Dar
es Salaam kupata adha kubwa ya usafiri kutokana na barabara kuharibika
na kulazimika Magari kuvutwa na Scaveta zinazofanya kazi ya kupunguza
mlima kinombedo uliopo wilaya ya Tandahimba.
Wakiwa katika jitihada
za kuvuka mlima Kinombedo ambao licha ya kuwepo kwa lami udongo
unaoporomoka kutoka juu ya mlima huo umekuwa ukisababisha utelezi na magari
kushindwa kupanda mlima ambapo awali madereva wanaoendesha mashine za
kuchimbia udongo walishindwa kutoa msaada na kulazimu madereva kuanza
kuchimba barabara hali ambayo ilisababisha foleni kubwa zaidi kutokana
na malori kuziba njia.
Baada ya jititihada zao kugonga mwamba na
kusababisha foleni ya malori ya mizigo pamoja na mabasi ya abiria,
Kampuni inayopunguza mlima chini ya msimamizi wake Bw. Haji Abubakari
ambaye hakutaka kutaja jina la kampuni inayofanya kazi ilitoa msaada wa
kuyavuta magari hayo ambayo baadaye yaliendelea na safari zake , Lakini
bwana Haji amesema eneo hilo linapunguzwa mlima ili kuwezesha magari
kupita kwa urahisi.
Wakiongea na Safari redio baadhi ya madereva
wanaofanya safari zao kati ya Wilaya ya Tandahimba, Newala na Dar es
Salaam wameilalamikia serikali ya Mkoa kwa kushindwa kujenga barabra
hiyo kwa kiwango cha lami licha ya kuwa imekuwa ina uhitaji mkubwa kwa
wananchi wanaoishi na wanaosafiti katika wilaya hizo.
Mmoja wa
madereva hao aliyejitambulisha kwa jina na Charles Paulo amesema mara
nyingi kipindi cha mvua kumekuwa kukijitokeza kero ya uharibifu wa
barabara ambayo kwa namna moja au nyingine imekuwa ikichangia uchakavu
wa vyombo vya moto ambavyo vimekuwa vikipita katika barabara hiyo.
Wiki iliyopita Serikali kupitia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ilisema imetenda fedha zaidi ya shilingi Milion 1000 kwa ajili ya
kukarabati miundombinu ya barabara na kujenga kwa kiwango cha lami
barabara inayounganisha Mkoa wa Mtwara na Viunga vyake.Kuhu ikidai kuwa
serikali kupitia wakala wa barabara Tanroads tayari imesaini mkataba na
mkandarasi kutoka Botswana.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni